HIZI NI SALAMU ZA BONDI KWA DORICE WA COSOTA

I kiwa zimepita siku kadhaa tangu rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aagane na wasanii wa nchini Tanzania na kutoa maagizo kadhaa ikiwamo suala la kufuatilia mirahaba na haki za wasanii, msanii wa filamu nchi Bond ameamua kutuma salamu kwa Dorice wa Cosota ambaye atakuwa mfuatiliaji.

Bond87

Jamani naombeni mnifikishie salam zangu kwa dada Doris wa Cosota

Jana usiku wa tar 6/08/2015 kwa mara ya kwanza nadhani alijikuta anasimama pembeni ya rais wa jamhuli ya muungano Mh. JK na kujibu maswali magumu kwa njia nyepesi tu.

Amepewa muda wa wiki mbili kukamilisha ripoti ya masuala yetu wasanii yakiwemo ya mirabaha na mengineyo ya wazi wa kazi na masuala ya haki.

Kwanza nimpongeze sana kwa anavyojitahidi lakini kikubwa zaidi nisisi kama wasanii tunaomba awe muwazi kabisaa katika ripoti yake kuwa

COSOTA haina ofisi ya kudumu,

COSOTA haina ghala la kuhifadhia mali zinazokamatwa baada ya misako na hii inasababisha wasifanye misako ya kukamata,

COSOTA haina sheria ya kutoza mirabaha kwa wadau bali inawaomba wachangie tu na unapomuomba mtu basi ujue ana hiari ya kutoa anacho jisikia au asitoe kabisa,

COSOTA haina ofisi mikoani

COSOTA haina wafanyakazi wa kutosha,

COSOTA ina gari moja tu je linaweza kuzunguka nchi nzima?

COSOTA inatakiwa ipate asilimia katika pesa za stika za kwenye CD ili iweze kufanya misako ya kazi feki na wizi la sivyo haina haja ya kuweka stamp za TRA na tuweke Stamp za Cosota

Pia COSOTA isimamie haki ya kazi za wanachama wake kikamilifu

Haina haja ya kumuomba mkaguzi wa hesabu wa serikali ili akaikague kosota kuwzia mwaka 1991 mpaka sasa na kujua imeingiza kiasi gani kupitia mirabaha ya sanaa ya mziki na filamu kuanzia Mabar, Mahotel, Mabasi, vituo vya Tv, vituo vya redio, kwenye mameli, ndege, libraly, cable netwok, vibanda vya video shows na sehem nyinginezo na imetoa kiasi gani kwa wahusika bali hivi sasa tunaomba tuanze mwanzo mpya kabisa

Huu ni wakati wa kusema ukweli ili nasi tule halali yetu ukificha ficha tena hali mbaya sana inakuja na mungu ndio atakae tusaidia kuyaweka bayana na yakiwa bayana itakuwa aibu kubwa sana kwa Cosota

Hizi ni salamu zangu nifikishieni jamani

Naitwa Bond 

Wastara Juma on instagram

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s