MR. BLUE: WATOTO WANATAKIWA WALALE BABA NARUDI KWENYE GAME

Msanii Khery Sameer Rajab maarufu kama Mr Blue amefunguka na kusema sasa ni wakati wake kutoka kimuziki na kazi mpya baada ya kukaa kimya takribani kwa miaka mitatu tangu alipoachia wimbo wake ambao uitwao ‘Pesa’

Mr%20Blue_0

Mr Blue kupitia katika mtandao wa Instagram amewashukuru mashabiki wake kwa uvumilivu wao vile ambavyo wamekuwa wakimsubiri kwa muda wote huo ambao alikuwa kimya baada ya kuachia wimbo wake wa mwisho ambao bado unafanya poa mpaka sasa.

Mbali na hilo mkali huyo amewatahadharisha wasanii wenzake ambao walikuwa wakitamba katika soko la muziki muda ambao alikuwa kimya kuwa wakae sawa kwani muda wake kurudi na kufanya kazi umewadia, hivyo wanalazimika kumpisha maana amedai wamecheza sana na muziki.

“Nawashukuru sana wadau wangu wa kazi zangu…kazi inakuja kazi mpya kutoka kwa kijana wenu imefika takribani miaka mitatu sasa tangu nilipotoa wimbo wangu wa mwisho ‘Pesa’ ambao mpaka leo bado upo namshukuru muumba aliyenipa kipaji cha kutengeneza nyimbo zinazodumu, watoto wameshacheza sana muda wao wa kwenda kulala umefika nafikiri wote mnajua kuwa watoto wanatakiwa kulala mapema hasa baba anapokuwa amerudi,” alisema Mr Blue.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s