CHRISTIAN BELLA ATOA YA MOYONI KUHUSU WASANII WA BENDI

Mwanamuziki na mmiliki wa kundi la Malaika Band Christian Bella maarufu kama Mfalme wa Masauti amewatolea uvivu wanamuziki wa bendi ambao ni washindi wa tuzo mbalimbali katika Tuzo za Kilimanjaro Music Award na kuwapa shavu wasanii kutoka kundi la Yamoto Band.

Bella%20

Christian Bella wiki iliyopita alikuwa akifanya show katika mikoa ya nyanda za juu kusini kufuatia muamko wa mashabiki ambao walikuwa wakijitokeza kumpa support ndicho kitu kilichofanya kujiuliza mambo kadhaa juu ya wamanuziki wa dansi ambao walioshinda tuzo mbalimbali mwaka 2014.

“HIvi leo nimejuuliza wasani wenzangu wa live band wanaoshinda tuzo mara wimbo bora, mara mwimbaji mara mtunzi bora, mara band bora mbona sijawahi kuona wala kusikia nyimbo zao zikifanya vizuri nakupata shangwe kwenye show na mitaani ???” aliuliza Christian Bella

Kufuatia suala hili ndipo hapo mkali huyo wa masauti alipotoa pongezi kwa vijana wa band kizazi kipya kundi la Yamoto Band ambao wamekuwa wakifanya vizuri mitaani na hata katika show zao mbalimbali kwa kupata muamko mkubwa kwa mashabiki na nyimbo zao kupendwa sana mtaani na watoto na watu wazima.

Mbali na hilo Christian Bella amesema ndani ya mwezi huu anategemea kutoa video mbili tofauti, Video ya kwanza ya wimbo ‘Amerudi’ ambao amefanya yeye pamoja na Malaika Band itaanza kutoka tarehe 21 huku Video na Audio ya wimbo ‘Minamgharamia’ ambayo amefanya na Ali Kiba inatarajiwa kutoka mwisho wa mwezi huu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s