JUX: JOH MAKINI HAJAWAHI KUSHUKA KWENYE SANAA

Msanii Juma Jux ambaye ni mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa RnB (2014) katika tuzo za Kilimanjaro Music Award ameonyesha mapenzi yake na kukubali kiwango cha rapa kutoka katika kundi la Weusi, Joh Makini

jOH%20mAKINI%20

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkali huyo wa RnB amesema wakati anaanza kufanya kazi ya muziki alikuwa anavutiwa sana na kazi zake na tangu amemfahamu anakiri wazi kuwa hajawahi kuona ameshuka katika viwango vyake vya muziki bali anazidi kufanya poa siku hadi siku na kuzidi kuwa bora zaidi.

Jux amesema kutokana na Joh makini kufanya kazi bora kila siku maanimi kuwa ndio maana watu walimpa jina la Mwamba wa Kaskazini.

“Kipindi naanza muziki nilikuwa namsikia tu Joh Makini na nakuvutiwa sana na kazi zake. Na tangu namfahamu mpaka sasa hajawahi kushuka ni kupanda tu kwenye sanaa, I guess that’s why they call him Mwamba,” alisema Jux.

Wakali hao wawili wamekutana katika kazi moja ambayo inakwenda kwa jina la ‘Nakutafuta’ Looking for you’ ambayo ni kazi ya Jux akimshirikisha Joh Makini na video ya wimbo huo umefanyika Afrika Kusini na mwongozaji video Justin Campos.

Jux anasema alishukuru sana baada ya mkali Joh Makini alipokubaliana na ombi lake la kufanya kazi pamoja na kuweza kuweka mistari mikali katika wimbo huo ambao kwa mara ya kwanza umeaanza kuonekana katika vituo vya Luninga vya kimataifa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s