MAJIMBO MATANO KURUDIA KUPIGA KURA ZA MAONI CCM

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi katika majimbo matano yaliyopo Tanzania Bara kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.

Nape-Nnauye_1

Majimbo yanayotakiwa kurudia uchaguzi wa kura ya maoni ni pamoja na Makete, Busega, Ukonga, Rufiji na jimbo la Kilolo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya Alhamisi Agosti 13 mwaka huu.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.

Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea katika ukumbi wa NEC mjini Dodoma amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.

Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha Kamati Kuu ambapo kesho na kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho (NEC) kama ilivyopangwa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s