NAY WA MITEGO AELEZA VITU ANAVYOVIPENDA SANA

Msaniii wa Bongofleva Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake siku zote anapenda vitu viwili kikiwepo kuangalia movie (filamu) na pili kushiriki tendo la ndoa na mtu wake wa karibu.

Nay

Nay wa Mitego aliyasema hayo jana alipokuwa akipiga stori katika kipengele cha stori tatu ya Planet Bongo, mkali huyo anasema yupo radhi hata asile chakula kama akiwa anaangalia Movie ambayo anaipenda na kusisitiza kuwa pia anapenda sana kufanya mapenzi kama ambavyo amekiri katika wimbo wake mpya wa ‘Sina Muda’.

“Mimi napenda sana Movie kweli napenda sanaa movie yaani kama kuna Movie nafuatilia halafu ninaipenda unaweza kuniwekea chakula pale lakini nitasahau kula, ila pia napenda sana kufanya mambo ya kujamiaaana na mtu wangu wa karibu, kweli kabisaa nimeimba kwenye wimbo wangu mpya, napenda sana kitendo hicho,” alisema Nay wa Mitego.

Mpaka sasa Nay wa Mitego ni baba wa watoto watatu ambao kila mmoja ana mama yake na hii inaweza kuthibitisha kauli yake ya kupenda sana mapenzi.

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s