HII NDIO TAREHE YA TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO MWAKA HUU …..

Tamasha la Sanaa na utamaduni Bagamoyo mwaka huu litafanyika kwa mara ya 34 kuanzia tarehe 21-27 septemba katika ukumbi wa viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe.

DSCN1114

Tamasha la mwaka huu limebeba kauli mbiu Isemayo “SANAA NA UTAMADUNI KATIKA UCHAGUZI HURU NA WA AMANI” aidha kutakuwa na Mada ndogondogo zitakazotolewa kupitia kongamano na warsha zitakazohusu haki za binadamu, rushwa na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)

Katika tamasha la mwaka huu litausisha ngoma za asili, maigizo, sarakasi, mazingaombwe, muziki wa kisasa na asili, Sanaa za ufundi na bidhaa mbalimbali.

Tamasha la Kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Lengo Kuu la tamasha kwa wakati huo ilikuwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha Sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliyojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, Baada ya tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa chuo uliamua tamasha lifanyike kila mwaka kwa vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya nchi kubadilishana uzoefu na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.

Written By #Dauka Somba

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s