UJUMBE KUTOKA KWA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN

Kundi la kigaidi la A Qaeda limetoa ujumbe wa sauti ambao unadai kwamba umetoka kwa Hamza Bin Laden ,mwana wa Osama Bin Laden.

 141106221249_sp_osama_bin_laden_promo_640x360_reuters

Ujumbe huo unaaminika kuwa wa kwanza wa propaganda za Al Qaeda kumshirikisha Hamza Bin Laden kama mwanachama wa kundi hilo.

Katika ujumbe huo uliosambazwa na Al Qaeda katika mtandao wa twitter,Hamza Bin Laden anaagiza mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake.

Osama bin Laden aliuawa na vikosi maalum vya Marekani mnamo mwaka 2011 katika uvamizi nyumbani kwake huko Abbotabad,Pakistan

wanajeshi maalum wa Marekani wakati walipovamia makaazi ya Osama Bin Laden huko Pakistan

Kundi hilo limekuwa likiongozwa na naibu wake Ayman al-Zawahiri.Uwepo wa Hamza Bin Laden haujulikani,anadaiwa kuwa mwenye umri wa miaka ya 20.

Wakati wa uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2001,shirika la habari la Al-Jazeera lilionyesha picha yake miongoni mwa wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

Ujumbe wake wa sauti uliotolewa na Al Qaeda unawataka wafuasi wake mjini Kabul,Baghdad na Gaza kuanzisha jihad ama vita vitakatifu mjini Washington,London,Paris na Tel Aviv.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s