JOKATE: WAZAZI WASIINGILIE MAPENZI YA WATOTO

SIKU chache baada ya gazeti la Ijumaa Wikienda kuripoti juu ya wazazi wa Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumkataa Ali Kiba kama mchumba wake, binti huyo ameibuka na kuwataka wazazi kote nchini kuacha kuwaingilia watoto wao katika masuala ya kimapenzi, akidai jambo hilo ni vema wakiachiwa wenyewe.

11910136_147181532285484_807925537_n

Kwa mujibu wa gazeti la Ijumaa, Jokate alisema ni vyema kama wazazi wakawaacha watoto wao waoe au kuolewa na watu wawapendao, kwani vinginevyo ni kuwaingilia maisha na uhuru wao binafsi, jambo ambalo si jema.

“Unajua nimelala, madai ya Ally (Kiba), sitaki kuyazungumza sana, unajua mimi ni binti mtu mzima, ninao uhuru wa kumchagua nimpendaye kwa ajili ya maisha yangu, ifike mahali wazazi wawape uhuru watoto wa kufanya mambo yao, awamu hii siko tayari kuona naumizwa tena na familia juu ya uhusiano wangu,” alisema binti huyo kwa njia ya simu juzi.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s