UKAWA NA CCM WAZINDUA KAMPENI

Wapinzani wawili wakuu katika uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania wamezindua kampeini zao rasmi.

150712095247_ccm_je__dr_john_magufuli__ndiye__624x351_bbc_nocredit

Uchaguzi ujao licha ya kuwa na wawaniaji kiti cha urais wengi umeibuka kuwa na ushindani mkubwa kati ya chama tawala cha CCM na kile cha upinzania Ukawa.

Washindani wakuu ni mwakilishi wa chama tawala, Chama cha mapinduzi CCM,daktari John Magufuli na mpinzani wake ambaye alikuwa ni waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa ambaye anapeperusha bendera ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

150810144207_lowassa_640x360_bbc_nocredit

Huu ndio uchaguzi wa tano tangu kurejea kwa utawala wa vyama vingi vya kisiasa.

Uchaguzi wenyewe umeratibiwa kufanyika Oktoba tarehe 25.

Hii ndio mara ya kwanza tangu kujinyakulia uhuru mwaka wa 1961, ambapo chama tawala cha CCM kinakabiliwa na upinzani mkubwa zaidi.

Chama hicho, kimeathirika zaidi na kuhama kwa vigogo wa chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani kutokana na uhasama ndani ya chama.

Kuhama kwa waziri mkuu wa zamani Lowassa, ambaye alikuwa amepigiwa upatu kutwaa tikiti ya kuiwakilisha CCM katika uchaguzi ujao kumeibua hisia kali miongoni mwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano yake ya hadhara.

150823111401_pande_zote_zinabashiri_kuwa_zitapata__ushindi_mkubwa_512x288_bbc_nocredit

Licha ya kudhaniwa kuwa na ushawishi mkubwa, bwana Lowasa na muungano wa Ukawa unakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa chama cha mapinduzi ambacho kinaufuasi mkubwa mashinani

Pande zote zinabashiri kuwa zitapata ushindi mkubwa.

Profesa Kitila Mkumbo anasema kuwa hii ndio mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 ambapo chama cha CCM kimegawanyika katikati.

”Kwa hakika hii ni uchaguzi kati ya CCM ya Magufuli na CCM ya Lowassa.”

‘Wote wamekuwa katika CCM,Lowasa anakumbukwa kwa kuleta mabadiliko ndani ya chama ,mabadiliko ambayo yameisaidia chama kuendelea kuwa na ufuasi sugu mashinani”anaongezea Profesa Kitila.

‘Iwapo mtu atadhania kuwa ufuasi tunaouona ndani ya Ukawa kufuatia kujiunga kwa Lowassa ni ufuasi hewa, basi na ataadhari maanake asingelikuwa na wafuasi kote aendako’ Profesa Kitila aliiambia runinga ya EATV.

Hoja yake hata hivyo inapingwa na viongozi wakuu wa CCM wakiongozwa na rais anayeondoka Jakaya Kikwete.

Wao wanashikilia hoja kuwa CCM itashinda bila wasiwasi wowote na ninajua wapinzani wetu watashangaa hapa , CCM itafunga magoli mapema tu wao wakiwa wameganda wamepigwa na butwaa” alisema Kikwete.

Upinzani tayari umellamika kuwa polisi na vyombo vya usalama vinatumika kuwahujumu.

150730120439_lowassa_tanzania_640x360_bbc_nocredit

Mgombea wa Ukawa, Lowassa aliwakashifu kwa kuwazuia wafuasi wake waliojitokeza kumpokea alipokwenda majimboni.

Lowassa alivutia umati mkubwa wa watu alipozuru Mwanza Arusha , Zanzibar na hata mji mkuu wa Dar es Salaam.

Wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanasema kuwa wandani wa CCM sharti wazingatie umaarufu wa Lowassa wanapoanza kampeini zao na sharti wanadi sera zao kwa kutumia mbinu kabambe ikiwemo kujumuishwa kwa mwanamke bi Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza wa daktari Magufuli.

Hayo yote ni kenda wapiga kura wenyewe nao hawana budi kuwasikiliza wagombea urais kwa umakini sana iliwaweze kubaini kiongozi yupi atawafaa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s