wananchi wanatakiwa kushiriki uchaguzi kwa amani

Raia nchini Tanzania wametakiwa kujiepusha na vitendo mbalimbali ambavyo vinaweza kuchochea uvunjifu wa Amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.

CIMG7789

Kauli hiyo imetolewa leo jijini la Dar es salaama na kiongozi mkuu wa taasisi ya Global Peace Foundation nchini Martha Nghambi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Amani kwanza yenye lengo la kuwahamasisha wananchi hususani vijana kuwa mabalozi wa Amani katika kipindi hiki.

Nghambi amesema kauli mbiu ya kampeni hiyo ni KURA YANGU UZALENDO WANGU, AMANI YA NCHINI YANGU NI JUKUMU LANGU. ambayo imeandaliwa na taasisi hiyo yenye makao makuu yakee nchini marekani ambayo inahsmasisha Amani duniani kote.

CIMG7782

“Kampeni hii haina lolote la kuunga mkono chama chochote cha kisiasa au mgombea wake wala haina mahusiano ya kisiasa pia ili kuhakikisha tunafanikiwa tutashirikiana na vyombo vya habari pamoja na wadau mbalimbali”, alisema Nghambi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa baraza la dini mbalimbali la Amani nchini Thomas Goddas amesema wanashrikikiana na taasisi hiyo ili kuwahimiza wagombea kuwachanganulia wananchi kwamba watanufaika vipi kupitia rasilimali zilizopo pamoja na kuboresha sekta muhimu kama Elimu, ajira pamoja na kilimo.

Written By Dauka Somba

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s