Lowassa aanza Iringa,Duni aacha mzozo Mtwara

Mgombea urais wa chama cha demokrasia na maendeleo Mh. Edward Lowassa akiambatana na waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye wameanza kazi ya kunadi sera zao mikoani katika mkoa wa Iringa huku wakiendelea kuungwa mkono na maelfu.

lowassa-3

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo mgombea urais huyo ameendelea kunadi sera za UKAWA na kuelezea azma yake ya dhati ya kufanya marekebisho makubwa na kwa wakati na kuzisimamia kikamilifu.

Katika hatua nyingine Shinikizo kutoka kwa wananchi limepelekea mgombea mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juma Duni Haji, kulazimika kumtangaza Maftaha Nachuma wa Chama cha Wananchi (CUF), kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Mtwara mjini kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Maamuzi hayo yalitokana na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanywa na UKAWA jana katika viwanja vya mashujaa mkoani humo, kuwa na shauku ya kutaka kumjua mgombea wao.

Kwa upande wake, katibu wa kamati ya sheria na haki za binadamu wa CHADEMA kanda ya kusini, Hassani Mbagile, amesema wameyapokea maamuzi hayo kama yalivyoamuliwa na mgombea huyo lakini hayataishia hapo kwani watawasiliana na viongozi wa UKAWA ili kuhoji kama kuna uhalali wa mgombea kutoa maamuzi kutokana na shinikizo kutoka kwa wananchi.

Kwa upande wake, mgombea wa NCCR Uledi Hassan, alipotafutwa na East Africa Radio kuzungumzia maamuzi hayo alisema hawezi kuzungumza chochote kutokana na kuwa

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s