Marehemu Shreekezy kusafirishwa Kenya kwa Maziko

Jitihada za kumsafirisha aliyekuwa aliyekuwa mdau wa burudani na rapa marehemu Shreekezy, kwenda huko nchini Kenya kwaajili ya maziko, zinaendelea kufanyika kupitia michango mbalimbali ambayo inakusanywa kupitia kundi la Navy Kenzo.

aaa_0

Hii ni baada siku ya jana marehemu kupatikana mwili wake ukiwa umeharibika vibaya baada ya baada ya kupotea kwa takriban siku tatu katika kisiwa cha Mbudya kilichopo bahari ya Hindi Jijini Dar es Salaam.

Kifo cha Shreekezy ambaye ni raia wa Kenya aliyekuwa anafanya kazi zake nchini Tanzania, kimewagusa watu wengi, hususan kwa karibu wasanii wa kundi la Navy Kenzo ambao kwa pamoja waliwahi kufanya kolabo wakijulikana kama Pah One, kazi iliyofanya vizuri inayokwenda kwa jina “I Wanna Get Paid”.

Msanii wa muziki Meninah pia ni moja kati ya watu wa karibu ambao wanaguswa na msiba huu wakijaribu kujipanga kuhakikisha kuwa wanafanya kila kinachowezekana kuweza kumsafirisha marehemu mpaka kwao kwaajili ya maziko.

ddd_3

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s