Mwongozaji wa Tylor Swift atetea video

Mwelekezi wa video mpya ya Taylor Swift iliyoshutumiwa kwa kuonyesha picha mbaya ya Afrika amejitokeza na kuitetea vikali.

150903144817_taylor_swift_clip_africa_640x360_universal

Video hiyo ya wimbo Wildest Dreams imedaiwa kuendeleza dhana potovu ya maisha bora iliyokuwa na wakoloni barani Afrika.

Lakini mwelekezi Joseph Kahn amesema “video hiyo haihusu ukoloni bali ni simulizi ya kisa cha mapenzi katika kundi la waandalizi filamu Afrika, 1950”.

Swift hajazungumzia utata uliogubika video hiyo.

Kupitia taarifa, Kahn amekanusha madai kwamba video hiyo imeshirikisha Wazungu pekee.

“Ukweli ni kwamba sio tu kuwa kuna watu wa asili nyingine kwenye video hiyo, bali pia wabunifu waliofanyia kazi video hiyo ni wa asili nyingine.”

Ameeleza kuwa yeye ni wa asili ya Asia na Amerika, naye produsa wa video hiyo Jill Hardin na mhariri Chancler Haynes ni Waafrika Waamerika.

“Tuliamua kwa pamoja kwamba haingekuwa sahihi kihistoria kujaza waigizaji weusi kwenye video hiyo kwani tungeshutumiwa na kudaiwa kujaribu kuandika upya historia.

“Video hii inaonyesha mambo ya zamani kupitia watu wanaoishi kwa sasa na tunajivunia kazi yetu.”

“Kuna Waafrika weusi kwenye video hiyo, lakini sikuangazia sana watu wengine kwani muda mwingi unachukuliwa na Taylor na Scott (Eastwood).”

Video hiyo imetazamwa mara milioni 22 tangu ipakiwe mtandaoni Jumatatu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s