SHERIA YA MTANDAO YAFAFANULIWA NA TGNP

WIZARA ya sayansi,teknologia na mawasiliano kwa kushirikiana na TGNP MTANDAO waliopo mabibo jijini Dar es salaam,wameendesha warsha ya sheria ya makosa ya mtandao na miamala ya kielektroniki kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuanzia ngazi ya kijamii mpaka ngazi ya kitaifa na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii kutoka maeneo tofauti nchini.

 Screenshot_2015-09-03-18-42-14 [244305]

Katika warsha hiyo wizara ya mawasiliano iliwasilishwa na wanasheria wake watu VERONIKA SUDAYI,UNICE MASIGATI na ANNA KALOMO na kueleza kuwa sheria hii ni utekelezaji wa sera ya Tehama(teknolojia na mawasiliano) ya mwaka 2003,huku mchakato wa utekelezaji ukianza rasmi januari 28 2013

 Akizungumza kwenye warsha hiyo Masigati alisema kuwa sheria hiyo adhibu inaainisha adhabu na makosa ya kimtandao kama kuingilia mifumo ya mawasiliano bila ruhusa ya mhusika,kutoa taarifa zisizo sahihi,wizi wa mtandaoni,kusambaza picha chafu  na kusambaza jumbe zenye kuchochea chuki au kupotosha jamii pia alitaja baathi ya faida za sheria hiyo kuwa ni pamoja na kulinda taarifa binafsi kwenye benki,mamlaka za uhamiaji,hospitali na pia kwenye manunuzi ya bidhaa au huduma  mtandaoni,sheria hiyo pia imeanza kutambua miamala ya kielektroniki na mfumo wa serikali mtandao (E-GOVERNMENT)

 Waandishi wa habari wameiomba serikali kutoa elimu kwa jamii njuu ya sheria hiyo kwani jamii imeingiwa na hofu tangu kuanza kwa utekelezaji wa sheria  pia serikali iboreshe changamoto mbalimbali zilizopo katika sheria hiyo.

Written By Patson Kalinga

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s