Wanenguaji wawili wafungwa jela Misri

Mahakama nchini Misri imewahukumu wanenguaji viuno wawili kufungwa jela miezi sita kila mmoja kwa kuchochea uasherati.

 140903181024_belly_dancer_512x288_bbc

Suha Mohammed Ali na Dalia Kamal Youssef, wanaojulikana kama Shakira na Bardis wa Misri, walikamatwa kwa kusakata ngoma katika video wakiwa nusu uchi.

Mawakili waliwasilisha malalamishi kortini, wakisema wawili hao walikuwa kero kwa umma kimaadili na waliwaharibia sifa wanawake wa Misri.Mwezi Machi, mchezaji densi mwingine kwa jina Safinaz alifungwa jela miezi sita kwa kuikosea heshima bendera ya taifa hilo.

Alikuwa ametokea kwenye video akivalia nguo yenye rangi za bendera ya Misri.

Msakataji densi mwingine, Salma el-Fouly, alifungwa miezi sita mwezi Julai kwa kucheza kwenye video akiwa amevalia mavazi mafupi na kuonekana kuchezea waume.

Mwanamume aliyepiga picha hizo za video pia alifungwa jela miezi sita, huku mwanamume wa pili aliyetokea kwenye video hiyo na ambaye pia alihudumu kama produsa akihukumiwa mwaka mmoja jela bila yeye kuwa kortini.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s