Siasa isitugawe wasanii :Ray Kigosi

Msanii wa tasnia ya filamu nchini Ray Kigosi amewataka wasanii kutogawanyika na kuvunja umoja sababu ya ushabiki wa siasa na maslahi ya watu wachache bali wasimame pamoja kwa maslahi mapana ya taifa.

Ray%20Kigosi%20

Ray aliyasema hayo jana kupitia Ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliandika “Kumekuwa na kundi la wasanii ambalo moja kwa moja limekuwa likitoa support kwa wagombea wa nafasi ya urais na kuwataka wananchi kumchagua kiongozi fulani kwa kuwaaminisha ndiye kiongozi bora zaidi ya mwingine,” jambo ambalo Ray Kigosi analipinga na kuona si sahihi kwani anaona ni upotoshaji mkubwa.

“Kwenye uchaguzi wa mwaka huu nimewajua baadhi ya wasanii waliokuwa na akili na wasiokuwa na akili japokuwa nami nawezakuwa mmoja wapo katika hao wasiokuwa na akili. kwanini nasema hivi na samahani kama nitakuwa nimetumia lugha kali, unajua nashanga sana sasa hivi kumekuwa na vita baina ya wasanii wanaosapoti (CCM) Na UKAWA, jamani siasa ni demokrasia kila mtu ana haki yakuwa upande anayeuona yeye unamfaa,” alisema Ray katika ukurasa wake huo.

Kufuatia tofautui hiyo Ray aliwakumbusha wasanii kazi yao kubwa ni sanaa na si kufanya siasa na kuwataka kuwa makini na watambue kuna maisha baada ya Uchaguzi Mkuu na pia kutumia nafasi yao sasa kuwakumbusha viongozi umuhimu wao kama wasanii.

“Mimi nilidhani badala ya kuwa na tofauti nilitegemea kuwa tungekaa pamoja nakujua madhaifu ya chama na chama gani kitatufaa ili kiweze kutusaidia maslahi yetu pamoja na maslahi ya wananchi wanaoishi maisha ya tabu kwenye nchi yenye kila aina ya utajiri badala yake tunapambana wenyewe kwa wenyewe ?,” alihoji Raya na kuongeza jamani wasanii mmesahau shida zetu zote kwa kipindi hiki kifupi cha uchaguzi kumbukeni siasa si kazi yetu kazi yetu ni sanaa tusiwe wajinga huu ndio wakati wa kuwafunza viongozi waliokuwa wanaidharau tasnia ya sanaa na wananchi waliokuwa wakiwaona ni sawa na box lisilo na bidhaa ndani yake najua wasanii wenzangu kwamba kipindi hichi ni cha mavuno lakini tuangalie tusije tukala mpaka mbegu na kuzipata tena mbegu zingine mpaka miaka mitano ijayo”.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s