Play Back haziwezi kututoa kimataifa -Peter Msechu

Msanii Peter Msechu amefunguka na kuwatolea uvivu wasanii ambao wanapata nafasi kufanya shoo za kimataifa halafu wanafanya shoo hizo kwa mazoea na kushindwa kufikia kiwango cha kimataifa jambo ambalo linazidi kudidimiza tasnia ya muziki wa Bongo.

Msechu%20_0

Msechu amewataka wasani wa Bongo kutumia vyema nafasi ambazo wanapata kufanya shoo nje ya taifa, kuhakikisha wanazifanya kwa weledi na ubunifu wa hali ya juu na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.

“Kuna kitu kimoja sisi wasanii wa kibongo tunakosea pindi tunapopata nafasi kwenda kufanya kazi nje ya nchi, wenzetu wanauelewa mkubwa wa muziki hivyo tunashukuru watanzania wanaoishi nje ambao huwa wanaanda matamsha nje, lakini tatizo lipo kwa wasani wenyewe mtu anakwenda Ulaya halafu anapiga play back, yaani unakuta mtu anafanya shoo kawaida sana kama yupo Tanzania jambo ambalo linafanya hata watu ambao wanajua muziki kushindwa kuwasaidia wasanii hao kutokana na uwezo wao ambao wanakuwa wameonyesha katika shoo hizo,” alisema Peter Msechu

Mbali na hilo Msechu amesema imekuwa kawaida kwa wasanii ambao Tanzania wanadharaulika kama wale ambao wanafanya muziki wa Segere na aina nyingine ya muziki ambao unaonekana kama wa kishamba Tanzania ndiyo wanaofanya vizuri ugenini kwa sababu wanakuwa wanafanya kitu ambacho kwa wenzetu kinakuwa ni kigeni, tofauti na wasanii wa Bongofleva ambao wanafanya vitu vile vile kila siku bila kuwa na ubunifu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s