Sheria ya makosa ya mitandao itatuumiza: Bonta

Msanii kutoka katika kundi la Weusi Bonta Maarifa amesema sheria ya makosa ya kimtandao itatuumiza watanzania wengi kutokana na watu wengi kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya sheria hizo.

Bonta ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, ambapo amesema watanzania wengi wamekuwa watu wa kuanza kutukana, au kutumia lugha za kuudhi na kuhukumu vitu kwenye mitandao pasipo kusoma wala kufahamu hicho kitu kiundani wake, jambo ambalo anaona linaweza kuwaumiza watu wengi ambao hawana uelewa wa kutosha juu ya sheria mpya ya makosa ya kimtandao ambayo imeanza kutumika rasmi tarehe 1 mwezi huu.

“Hii sheria ya uhalifu wa makosa ya kimtandao itatuumiza watanzania, unajua tumekuwa na tabia ya kuhukumu vitu kwenye mitandao bila hata kufahamu mtu aliyeandika au kupost alikuwa na maana gani, wengine wanasoma tu kichwa cha habari na kuanza kutukana pasipo kufahamu umezungumzia nini, jambo ambalo linaweza sababisha watu wengi kutiwa hatiani, hivyo tunahitaji kueleweshana sana ili tusaidiane,” alisema Bonta Maarifa.

Tangu ianze rasmi kutumika kwa sheria ya makosa ya kimtandao hadi sasa hakuna kesi yoyote ambayo imefunguliwa au mtu kushtakiwa mahakamani kutokana na kuvunja sheria hiyo ya makosa ya kimtandao.

Chazo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s