Tanzania yapokea dola elfu 87 kwa ajii ya saratani ya mlango wa kizazi

Written By Dauka Somba

Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imepokea msaada wa dola za kimarekani elfu 87 kwaajili ya gharama za mradi wa matibabu wa wanawake wenye saratani ya mlango wa kizazi.

vC_-iplrxKGYGU_t3LGRcP2PmDH3LsvuW1bsET78QW4

akipokea msaada huo leo jijini Dar es salaam mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya ocean Road Beatrice Erasto amesema msaada huoutasaidia kuwasafirisha wanawake walio mikoani wenye ugonjwa huona kuwapeleka kwenye hospitali hiyo kwaajili ya matibabu ambapo mradi huo kwa kuanzia utahusisha mikoa ya Iringa, Mbeya na mwanza.

Amesema asilimia 25 ya wanawake wa Tanzania wako hatarini kupata saratani ya shingo ya kizazi katika maisha yao kutokana na asilimia 80 ya wagonjwa wanaogundulika kuwa na ugonjwa huwa katika hatua kubwa ambayo haina tiba wala kinga na hii zinaonyesha kwamba kati ya kila mwaka wanafikia 5000 wana tatizo hilo.

“serikali inafanya juhudi mbalimbali kupambana na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, juhudi hizi ni pamoja na kutoa elimu kuhusu aina mbalimbali za saratani na kuhakikisha kuwa vituo vyote vya afya vinapata vifaa vya uchunguzi na kutibu sratani,” alisema Erasto.

dPbT1qYqNfmz19mNyeA_Cwbhbxsd7Ulk7EEKyxHfAis

Naye mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Tanzania Marketing communication Diana kisaka amesema inakadiriwa kuwa kila mwaka wanawake Zaidi ya 6000 hugunduliwa na ugonjwa huo huku kati yao takribani 4000 huaga dunia kila mwaka ambapo ni sawa na wanawake 11 wanaofariki kila siku nchini kutokana na tatizo hilo.

nMS3LzU4JWvtQZCz6k4LqIMwKkZ9fHuPmh1rGXlqB-Y

Kwa upande wake mkuu wa mfuko wa Vodacom Renatus Rwehikiza amesema lengo la kampuni hiyo ni kuwasaidia wananchi kwa kuwafikia wanawake 1000 pamoja na kupunguza vifo kwa akina mama.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s