KALAPINA AHAIDI KUPAMBANA NA MADAWA KINONDONI

Mgombea ubunge jimbo la kinondoni kupitia ACT Wazalendo Karama Masoud (Kalapina) ameahidi kupambana na tatizo la madawa ya kulevya ambalo linaathiri vijana wengi katika jimbo la kinondoni.

12_0

Karama ameyasema hayo alipokuwa akizindua kampeni zake Katika soko la Tandale, baada ya kushinda kesi ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha CCM Iddy Azan.

Karama ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwanaharakati wa kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, amesema tatizo hilo limekuwa sugu kwa taifa zima, na linamaliza nguvu kazi ya Taifa.

“Ndugu wananchi baada ya kushinda pingamizi lililowekwa na mgombea mwenzangu, nipende kuwahakikishia mkinichagua mbunge wenu nitahakikisha tatizo la madawa ya kulevya linaisha katika Wilaya yetu kwani madawa ya kulevya yanamaliza nguvu kazi ya Taifa, kama nilivyoanzisha kipindi cha televisheni kuelimisha vijana wenzangu athari za matumizi ya madawa ya kulevya, ndivyo nitakavyoenda kulisemea kule bungeni juu ya uingizwaji wa madwa ya kulevya nchini uwe mwisho”, alisema Karama.

Pia Mgombea huyo amewataka wakazi wa kinondoni kufanya maamuzi ambayo yataleta mabadiliko kwa kuchagua viongozi watakaoenda kuwasemea matatizo yao, na si kupeleka watu wenye maslahi yao binafsi, ambao wanaenda Bungeni kuhakikisha biashara zao zinapita kwa urahisi kutokana na wao kuitwa Waheshimiwa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s