Wayne Rooney avunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton miaka 45 iliyopita

Wayne Rooney aliandikisha rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Uingereza alipofunga bao la 50 kupitia mkwaju wa penaltı dhidi ya Uswizi.

rooney

Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney atia wavuni mkwaju wa penalti katika mechi ambayo ataikumbuka milele. Bao ya Wayne Rooney ilivunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton miaka 45 iliyopita.Wayne Rooney alijitayarisha kupiga penalti katika dakika ya 84 baada ya Raheem Sterling kuchezewa visivyo katika eneo la hatari. Mashabiki kwenye uga wa Wembley walisubiria kwa hamu penalti hii ya kihistoria ambayo ingevunja rekodi ya miaka 45. Naye Wayne Rooney hakuwavunja moyo. Ulikuwa muda wa furaha na kihistoria kwa Wayne Rooney na kwa mashabiki wa soka wa Uingereza. Rooney ameweza kustahimili kashfa chungu nzima kufikia kiwango cha kuwa mfungaji bora wa Uingereza.

Kabla ya bao la kihistoria la Rooney, mshambuliaji wa TottenhamHarry Kane alikuwa ameiweka mbele Uingereza alipofyatua mkwaju katika dakika ya 67 baada ya kupoka pasi safi kutoka kwa Luke Shaw. Uingereza ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2 kwa nunge.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s