Picha, Floyd Mayweather amshinda Andre Berto

Bingwa wa ndondi katika uzani wa welter duniani Floyd Mayweather ameshinda pigano lake la 49 mfululizo kwa alama baada ya kumlemea Andre Berto mjini Las Vegas.

 150913080542_berto_mayweather_512x288_bbc_nocredit

Berto alikuwa moto lakini Mayweather, aliyekuwa akitetea mataji ya WBC na WBA katika uzani wa welter, alijikinga sana na kukwepa ngumi za Mmarekani huyo mwenzake.

Mayweather, 38, alizawadiwa alama 120-108, 118-110 na 117-111 kwenye pigano hilo lililoandaliwa ukumbi wa MGM Grand usiku wa kuamkia Jumapili.

 -775b7a74443dffd2

Mayweather amesisitiza kuwa hilo litakuwa pigano lake la mwisho, lakini ikizingatiwa kwamba amefikia rekodi ya Rocky Marciano ya kupambana na kushinda mapigano 49-0, huenda akaamua kuongeza.

“Maisha yangu ya uchezaji yamefikia kikomo, hilo ni rasmi,” alisema Mayweather ambaye sasa ni bingwa wa ndondi katika vitengo vitatu tofauti vya uzani.

Bondia huyo anachukuliwa sana na wengi kuwa stadi zaidi katika kizazi chake.

“Lazima ujue wakati wa kuacha. Sasa nakaribia umri wa miaka 40. Sijabaki na chochote cha kuthibitisha kwa ulimwengu wa masumbwi. Sasa nataka tu kufurahia maisha na familia yangu.”

Berto, 32, ni bingwa mara mbili wa dunia uzani wa welter na aliingia kwenye pambano hilo akiwa amewahi kupoteza mara tatu pekee katika mapigano 33 ya kulipwa aliyoshiriki.

Mayweather aliyekuwa akipigania ubingwa wa dunia mara ya 26 hajawahi kushindwa tangu 1996.

Iwapo ataamua kutostaafu, wengi wanatarajia huenda akaamua kukabiliana tena na Manny Pacquiao mwaka ujao.

Ukumbi mpya wa MGM utafunguliwa Aprili na pambano dhidi ya Pacquiao, ambaye Mayweather alimshinda Mei kwenye pigano lenye pesa nyingi zaidi katika historia, huenda likamvutia sana.

Aidha, anaweza pia akashawishika kukutana na mshindi wa pigano la Novemba 21 kati ya Miguel Cotto na Saul Alvarez.

-f37d50b0722ac6cb -b1e99295ab2575ad -5e83ba30a6e1e208

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s