Mourinho asema hajazoea kushindwa

Mkufunzi mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amesema anahisi jambo lisilo la kawaida, baada ya kilabu yake kukumbana na mwanzo mbaya zaidi wa ligi kuu katika miaka 29.

 150915151948_jose_mourinho_512x288_gettyimages

Mabingwa hao wa ligi ya Premier walilazwa na Everton Jumamosi, hiyo ikiwa mechi yao ya tatu kushindwa katika mechi tano walizocheza msimu huu. Matokeo hayo yamewaacha nambari 17 kwenye jedwali.

Vijana wa Mourinho watakutana na Maccabi Tel Aviv ya Israel mechi ya hatua ya makundi katika Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya Jumatano.

“Nawahakikishia kuwa niko salama,” alisema. “Sina raha. Sijazoea kushindwa mara nyingi hivyo lakini sasa nazoea hali hii.”

Akaongeza: “Huwezi kunitarajia niseme kila kitu kiko shwari, na kwamba kuna nicheko na mzaha. Watu wanapokosa ufanisi wanaopigania sana, basi watavunjika moyo.

“Tunajua kwamba sisi ni – mabingwa wa Uingereza. Mashabiki huimba hilo. Hakuna anayeweza kutupokonya ufanisi tuliopata kufikia sasa au vikombe tulivyoshinda au historia yetu, unaweza kujaribu lakini huwezi kufanikiwa.

“Unapozoea kushinda kila wakati, basi unapokosa kushinda unahisi jambo lisilo la kawaida. Baadhi hukabiliana na hali hii vyema, wengine hawawezi.”

Mourinho amesema hayo akihutubia wanahabari kuhusu mechi hiyo ya Jumatano dhidi ya Maccabi Tel Aviv.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s