ONE THE INCREDIBLE: NAIPENDA TAMADUNI MUZIK

Written by Dauka Somba

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harryson Kaale almaarufu kama One the Incredible amesema ukiachana na wazazi wake, mpenzi wake na watu wengine wa muhimu kwake, kitu kingine anachokipenda ni record label yake ya Tamaduni Muzik ambayo inahusisha wasanii tofauti tofauti na maprodyuza akiwemo yeye mwenyewe.

12002117_938319879589150_7163457218538136640_n

Kwa kudhihirisha hilo, One the Incredible amepiga tattoo katika mkono wake wa kushoto iliyoandikwa tamaduni Music, tattoo inayowakilisha kila kitu kinachomtafsiri yeye akiwa kama mmoja ya wasanii wanaounda crew hiyo na pia kama kumbukumbu katika maisha yake.

Msanii huyo amesema kuwa ni mara yake ya kwanza kuchora tattoo hiyo, na ni mwanzo tu wa nyingine zitakazokuja.

“Hii ni kumbukumbu ya kwanini mimi ni mimi na kwa nini nipo hapa kuendelea kufanya muziki na ninawapenda wazazi wangu kama ninavyopenda muziki pamoja na mpenzi wangu na watu wangu wengine wa karibu,” alisema One the Incredible ajulikanaye pia kama Moko Miujiza.

Kuhusu muziki wake, The Incredible ameongelea mapokezi mazuri ya albamu yake kwa mashabiki inayotambulika kwa jina la Represent Afrika Popote (RAP) aliyoitambulisha rasmi kwa wapenzi wa muziki mnamo Mei 12 mwaka huu, na iliyompatia tuzo ya Bronze kutoka kwa wasambazaji wa muziki mtandaoni waliopo nchini Kenya, mdundo.com kwa kufikisha downloads 50,000.

12039272_938318492922622_6814915813955290561_n

Kwa upande mwingine, Moko Miujiza aliongea kuhusu suala la uchaguzi na haki ya msingi ya kupig kura kw kuwaasa wale wote waliokidhi vigezo vya kupiga kura kufanya hivyo.

“Kama umefikisha umri wa kupiga kura huna sababu ya kwanini usipige kura. Nenda kampigie kura kiongozi unayemuhitaji. Kwa kutokupiga kwako kura utakuwa umemruhusu kiongozi usiyemtaka kuongoza dola.”

12032263_938321172922354_6636421860517108222_n

Mkali huyo amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wake kusubiri vitu vizuri kutoka kwake kwani mwaka huu amejipanga vilivyo ili kuweza kuhakikisha anadhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wa hiphop ambao wanautangaza mziki huo ndani nan je ya nchi

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s