JESHI LA POLSI, USALAMA BARABARANI LAANZA KATUMIA KANUNI MPYA,

Written by Dauka Somba

Jeshi la Polisi nchini kitengo cha usalama barabarani limeanza kutumia kanuni mpya za tozo kwa njia ya kielektroniki na kuweka nukta katika leseni za udereva.

 Mpinga

Akizungumza n waandishi waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Kitengo hicho Mohammedi Mpinga amesema kanuni hizo zitaanza kutumika September 17 mwaka huu ili kupunguza ajali za barabarani

Kamanda mpinga amezitambulisha mashine maalum ambazo zitatumika kwenye zoezi hilo na kuwataka wananchi wasiwe na shaka wakati watakapo waona askari wa usalama barabarani wakizitumia katika ulipishaji huo wa faini za papo kwa papo ambao utaanzia katika jiji la dar es salaam

“Nimatumaini yetu kuanzia na jiji la dar es salaam itatusaidia kubaini changamoto zitakazo jitokeza nakuweza kuja na mfumo bora Zaidi tutakapoanza nchi nzima,” alisema Mpinga.

Kuhusu suala la kuweka nukta katika leseni kamanda huyo amesema kadri dereva atakavyofanya makosa basi ataongezewa na zitakapofika kumi na tano atafungiwa kwa miezi sita.

Na ikumbukwe mnamo agosti 16 mwaka huu, kitengo cha usalama kilizindua kanuni za uwekaji viakisi mwanga katika vyombo vya usafiri.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s