Mbasha aachiwa huru

Mahakama ya Ilala Dar es salaam imemwachia huru mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma za ubakaji dhidi yake.

12049490_1324478317566583_413463843970058797_n

Akizungumza kwa njia ya simu na East Africa Radio, Mbasha amesema mahakama imefikia hatua hiyo baada ya kugundua hana kosa lolote, na anamshukuru Mungu kwa Ushindi wake huo.

“kwa kweli Mungu ni mkubwaamesikia kilio changu, na hatimae leo nimeachiwa huru, nimepitia kipindi kigumu sana kwa kweli, nawashukuru sana kwa kuniombea, kunifariji na kwa kunisapoti kwa kipindi chote nilichokuwa na matatizo”, alisema Mbasha.

Emanuel Mbasha alikumbwa na tuhuma hizo mnamo mwezi Julai mwaka 2014, na kesi yake kuendeshwa katika mahakama ya Wilaya Ilala ambapo leo ndio imetoa hukumu ya kesi hiyo.

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s