Vijana ni nguzo ya tamaduni za afrika

Written by Dauka Somba

Vijana nchini wametakiwa kujihusisha na masuala ya kitamaduni kwani kufanya hivyo kutaendelea kulinda hadhi ya Taifa na Bara la Afrika kwa ujumla

2-small

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kampuni ya ya Black Sensation Lilian Msuka amesema vijana na waTanzania ni nguzo muhimu kwenye kuendeleza utamaduni wa  mwafrika ambao hivi sasa umegubikwa na utanda wazi kwa kiasi kikubwa.

6-small

Masuka amesema hayo leo ambapo kwa kuliona hilo kampuni yake imeanda Tamasha la Fahari ya Mwafrika ili kuweza kuwaleta pamoja  raia nchini katika masuala ya maendeleo ya utamaduni, mila pamoja na desturi.

4-small

“Katika tamasha hili watu watajifunza mila na desturi za afrika na kuburudika kupitia muziki wa asili, maigizo ya vichekesho, mazingaombwe, lakini pia kutakua na vyakula vya asili na lengo letu kuwapatia watu nafasi ya kukumbuka mambo mbalimbali ya bara letu pia na kuwahamasisha vijana,”alisema Masuka.

Amesema Tamasha hilo litafanyika Oktoba 3 mwaka huu katika viwanja vya Escape One mbapo pia kutakuwa na vikundi vinne vya Sanaa, wabunifu saba  wa mavazi, bendi ya sky light pamoja na ile ya Barnaba classic.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s