Kajala Ammwagia Zari Minoti!

KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa picha hazipandi, staa wa filamu Kajala Masanja, mwishoni mwa wiki iliyopita alimmwagia ‘minoti’ mingi Zarinah Hassan ‘Zari’ wakati wa hafla ya kutimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwa mtoto wake Tiffah.

KAJALA56

Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Diamond, mitaa ya Madale-Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu.

Ilikuwa ni wakati Zari, alipokuwa akicheza muziki huku akipokea zawadi kutoka kwa waalikwa, ndipo muigizaji huyo, alipotumia zaidi ya dakika 20 kummwagia minoti ya shilingi elfu kumikumi. Baadhi ya watu waliohudhuria shughuli hiyo waliweka kipande cha video ya Kajala akifanya mambo yake kwenye mitandao ya intaneti na mara moja, Wema akakiona.

Inadaiwa kuwa kitendo hicho kilimkera na alipowasiliana na gazeti hili alisema. “Hata kama ni kweli tumegombana, bado yeye hakutakiwa kufanya vile, ilionekana anataka kunisanifu tu, kama kweli Kajala anasema kwa watu kila siku kuwa mimi ni rafiki yake na hawezi kuifuta tattoo yangu aliyojichora, asingeweza kufanya kitu kama hicho.

Sasa mwambieni kabisa kama ni hivyo, aifute mara moja ile tattoo,” alisema kwa kifupi, akionekana kukasirika. Risasi Mchanganyiko lilipomtafuta Kajala na kummegea ‘ubuyu’ huo, naye bila kupepesa macho alitiririka; “Mimi nilienda kumtunza Zari kama waalikwa wengine walivyofanya, kama yeye anaona sikufanya vizuri mimi hainihusu, na kama anaweza kuifuta hii tattoo aje tu aifute, haina shida.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s