Wasanii wa Kike Walio Katika Mapenzi na Wadogo Zao

Wengi wana sema umri namba mapenzi hayaangalia hilo sasa Kutana na wasanii wa kike nchuni tanzania ambao wanaishi na wapenzi wao ambao wamewazidi umri, hii ni kwa mujibu wa gazeti la mtanzania.

AUNTY5671

Aunt Ezekiel na Moze Iyobo

Mwigizaji wa filamu za bongo, Aunt Ezekiel, mwenye miaka 29, yupo kwenye mahaba mazito na Moze Iyobo, mwenye miaka 23, ambaye ni mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Kuzidiana huko kwa umri hakukuwafanya washindwe kuendeleza familia yao, kwa sasa wana mtoto mmoja. Aunt Ezekiel anasema: “Kitu muhimu katika uhusiano wetu ni mapenzi tunayopeana ambacho ndicho kitu tunachotaka katika uhusiano wetu na si suala la umri’’.

nuh-mziwanda1

Shilole na Nuh Mziwanda

Mwingine ni Zuhena Mohammed ‘Shilole’, ambaye ni mwimbaji na mwigizaji wa filamu za Bongo, naye amedondokea katika mapenzi ya msanii mwenzake, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

Umri wa Shilole ni mkubwa kuliko wa Mziwanda, lakini ukubwa wa umri huo hauwazuii kujivunia mapenzi yao na kufanya mambo yao mengine kama kawaida, ingawa mara kwa mara mashabiki wao wamekuwa wakiwapigia kelele kuhusiana na umri wao, lakini majibu ya Shilole ni kwamba; “Sikushawishiwa na mtu kumpenda Nuh Mziwanda, bali moyo wangu ndiyo ulimpenda na hakika ananidatisha siwezi kutengana naye kwa kuwa ni mwanamume kama walivyo wanaume wengine,” hayo ni maneno ya Shilole.

RIYAMA7761

Riyama Ally na Idd Mwalimu (Leo)

Mwigizaji mwingine ni Riyama Ally, huyu humwambii chochote kwa msanii wa muziki wa kufokafoka (hip hop), Idd Mwalimu Mzee, aliyemchumbia hivi karibuni.

Ingawa Riyama anadaiwa kumzidi mpenzi wake huyo kwa miaka saba, lakini umri huo haumkatishi tamaa mwigizaji huyo, ambaye muda wote amekuwa akiweka wazi kwamba wamepanga kufunga pingu za maisha.

Chanzo: Mtanzania

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s