MAN UNITED YAKAA KILELENI EPL NA MATOKEO YA MECHI NYINGINE.

Hatimaye Manchester United imekaa kileleni mwa ligi kuu England baada ya leo kuichapa Sunderland mabao 3-0 katika dimba la Old Trafford jijini Manchester.

12036984_1329187697095645_4507725254356003726_n

Manchester United imefikisha point 16 na kuipiku Manchester City ambayo leo imepigwa na Tottenham 4-1 na kubaki na point zake 15.

Katika mechi za leo , Liverpool pia imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa mabao ya Liverpool yakifungwa na James Milner dakika ya 2 na mengine yakifungwa na Daniel Sturridge dakika ya 59 na 67.

Arsenal pia imepata ushindi wa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Leicester City na kushuhudia Alexis Sanchez akirejea kwenye kiwango chake kwa kufunga mabao matatu (Hat-Trick) kati ya matano iliyopata Arsenal.

Nchini Hispania, Barcelona imepata ushindi wa maba 2-1 baada ya kuichapa Las Palmas katika dimba la Camp Nou, mabao yake yakifungwa na Luis Suarez dakika za 25 na 54 huku Neymar akikosa mkwaju wa penati dakika ya 67.

Mechi inayoendelea hivi sasa nchini humo ni Real Madrid Vs Malaga.

Mechi inayoanza saa 1:30 usiku huu, ni Chelsea ambayo iko ugenini dhidi ya Newcastle United.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s