Matokeo Ya Mechi ya Simba na Yanga, na mechi nyingine katika Ligi kuu Tanzania Bara.

Klabu ya Yanga leo imewapa raha wapenzi na mashabiki wake hii leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

12046666_1329140940433654_6289979664957014789_n

Mabao ya Yanga yamefungwa na Amis Tambwe dakika ya 44 na Malimi Busungu dakika ya 79.

Katika mchezo huo ambao timu zote mbili zilionesha dhamira ya ushindi, Simba iliyotawala zaidi kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi kadhaa ilizoweza kutengeza ikiwemo ile aliyopata Said Ndemla dakika za mwisho huku Yanga wakiweza kutumia nafasi chache walizopata kukwamisha mipira miwili wavuni.

Golikipa wa Yanga Ally Mustapha Bahtez aliweza kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa kupangua michomo kadhaa ya hatari kutoka kwa washambuliaji wa Simba wakiwemo Awadh Juma, Hamisi Kiiza na Mussa Hassan ‘Mgosi’

Katika mchezo huo pia, beki wa Yanga Mbuyu Twitte alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya manjano dakika ya 90.

Kwa ushindi huu Yanga imelipiza kisasi kwani katika mchezo uliopita Simba ikiwa haipewi nafasi, iliweza kuishinda Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi.

Yanga sasa imefikisha pointi 12 ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja, huku Simba ikibaki na point zake 9 kwa kushinda mechi 3.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo ni:

Coastal Union 0-0 Mwadui
JKT Ruvu Stars 0-1 Stand United
Tanzania Prisons 1-0 JKT Mgambo
Mtibwa 1-0 Majimaji
Kagera Sugar 0-0 Toto Africans

Kesho ni:-
African Sports Vs Ndanda FC
Azam Fc Vs Mbeya City.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s