Messi nje kwa majuma 8

Mshambulizi hodari zaidi duniani Lionel Messi wa Barcelona hatashiriki mashindano yeyote kwa majuma 8 yajayo kufuatia jeraha la goti.

 150926165747_messi_lesion_640x360_reuters_nocredit

Mshambulizi huyo wa Argentina aliumia katika mechi ya ligi kuu ya Uhispania dhidi ya Las Palmas.

Barcelona ilishinda mechi hiyo mabao 2-1.

Messi mwenye umri wa miaka 28 aliondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitalini kunako dakika ya 3 ya mechi hiyo.

Hata hivyo huenda mshindi huyo wa tuzo la mchezaji bora duniani akarejea katika mechi ngumu baina ya Barcelona na wapinzani wao wa jadi Real Madrid tarehe 22 Novemba.

Kocha Luis Enrique alisema kuwa atajitahidi kuendeleza mfumo wa mchezo wao hata bila ya messi kuwepo.

”Kutokuwepo kwa messi ni pigo ila tutalazimika kujifunga kibwebwe, na hili ninamaanisha kila mchezaji wetu atajikaza kisabuni ilikuziba pengo hilo japo ni kubwa…”

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s