Rihanna; Chris Brown ataingia Australia ?

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Marekani,Chris Brown ameonywa kuwa huenda asipewe ruhusa ya kuingia Australia kutokana na rekodi yake ya kumpiga mpenzi wake.

 150927104049_chris_brown_rihanna_afp_624x351_afp_nocredit

Brown alikuwa ananuia kwenda kuwatumbuiza mashabiki wake nchini humo mwezi December.

Mwanamuziki huyo ana siku 28 za kukata rufaa kwa afisi ya uhamiaji ya Australia.

Tiketi za shoo hiyo zilikuwa zimeratibiwa kuanza kuuzwa jumatatu (kesho).

Masaibu ya Chris Brown yanatokana na ripoti zilizochapishwa kote duniani mwaka wa 2009, kuwa alikuwa amemuzaba makonde mpenzi wake wakati huo Rihanna.

Japo amezuru taifa hilo mara mbili, shinikizo limejitokeza kwa serikali ta Australia kumnyima idhini ya kuingia.

Akitoa ilani ya kumnyima visa waziri wa uhamiaji wa Australia Peter Dutton alisema kuwa

”watu wanapaswa kufahamu kuwa mataifa mengine yanazingatia haki za wanawake kwa umakini na iwapo umewadhulumu wanyonge basi sharti ufahamu kuwa mataifa mengine yatakuadhibu”

150927103954_chris_brown_reuters_640x360_reuters_nocredit

Waziri wa maswala ya wanawake wa Australia Michaelia Cash,ambaye alikuwa naibu waziri wa uhamiaji hadi majuzi alisema kuwa waziri Dutton anapaswa kuvalia njuga swala la cheti cha kumruhusu brown kuingia Australia.

”Yafaa afahamu kuwa humu huwezi kuingia ilhali wewe huheshimu na kuwalinda watu wanyonge ikiwemo wanawake”

Wadau hata hivyo wanasema kuwa huenda hali imekuwa ngumu zaidi kwa Brown kufuatia kauli ya kumnyima bondia maarufu wa Marekani Floyd Mayweather ruhusa ya kuingia nchini humo mapema mwaka huu.

New Zealand tayari imemnyima hati ya kuingia nchini humo kwa tuhuma hizo.

Chanzo: tmz.com & bbcswahili.com

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s