TRA: VIKWAZO KWA WASAFIRISHA MIZINGO EA. HAVIPO TENA

Written By Dauka Somba

Mamlaka ya mapato nchini TRA imesema vikwazo vilivyo kuwepo katika usafirishaji wa mizigo kwenye jumuiya ya Afrika mashariki kwa sasa havipo tena kutokana na uwepo wa mfumo wa himaya moja ya forodha (single Customs Territory).

12059928_1934002326825144_9235706_o

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaa kamishina mkuu wa mamlaka hayo Rished Bade amesema mfumo huo ulioanzishwa juni 2014 utazihudumia nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kupunguza adha na kero zilizokuwepo awali.

Bade  amesema kama ilivyo kwa mataifa mengine ambayo ni wanachama wa jumuiya hiyo ambapo Tanzania na Rwanda zinatumia utaratibu wa ukaguzi wa nchimpokeaji (Destination Model of Goods) kama ilivyo kubaliwa na kupitishwa katika mkutano wa marais wan chi za Afrika Mashariki mnamo Novemba 2013.

“Utaratibu huu unawezesha mizigo kukaguliwa na afisa wa forodha wa Rwanda katika bandari ya Dar es salaam na kodi italipiwa Rwanda,” alisema Bade

Pamoja na mfumo huo  kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka nchini kwenda Rwanda Bade amesema changamoto zinazowakabili ni uchache wa elimu kwa wadau na wafanyabiashara pamoja na muingiliano baina ya masuala ya mitandao na uunganishaji wa mfumo huo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s