kuna maisha baada ya uchaguzi – Quick Rocka

Msanii Quick Racka amewataka wasanii kuwaachia wanasiasa kazi zao za siasa, na wao kubaki kuwa watoa burudani kwenye kampenina kuwakumbusha kuna maisha ya sanaa baad ya uchaguzi.

quick-rocka

Quick Racka ameyasema hayo kwenye Planet Bongo kipindi kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba kufanya kitendo hicho si kizuri kwao wasanii.

“Sijui kuna nini lakini naona kama wasanii wamejivika siasa ambayo sio kazi yao, kuna wengine ukiwauliza hawana hata kadi ya chama, ila wamejitwisha kitu ambacho sicho, wasisahau sisi kazi yetu ni sanaa na kuburudisha, mwisho wa siku hata kama umeitwa kwenye kampeni we kazi yako ni kuita watu na kuja kusikiliza sera za wagombea”, alise Quick Racka.

Pia Quick Racka amewataka wasanii wenzake kuacha kutupia vijembe wana siasa, wanapokuwa kwenye ajukwaa ya siasa na kampeni.

“Tusiende beyond that na kuanza kuwakejeli, si kitu kizuri, kama tunataka kutengeneza Tanzania yetu iendelee kuwa nzuri na amani, tufanye vitu fresh yani bila kutupiana maneno, hizo kazi wawaachie wana siasa”, alisema Quick Racka ambaye hivi karibuni amechia ngoma yake mpya ya nakupenda.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s