Nilimtumia mke wangu kwakuwa ana vigezo – Mabeste

Msanii ambaye anatarajia kuachia video yake baada ya kimya kirefu katika muziki Mabeste, amesema aliamua kumtumia mke wake kama video queen kwa sababu alikidhi vigezo vyote ambavyo director alivitaka, na ili aweze kujisikia vizuri na huru kwake wakati wa kazi.

Mabeste

Mabeste ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba alichokifanya pale ni sawa na kuhamishia kitu kutoka mfuko mmoja na kuweka kwenye mfuko mwengine.

“Unajua director wakati anaisikiliza nyimbo akawa anataka tu shoot, alikuwa anataka niwe na mwanamke ambaye ni mke wangu, kwanza nikajaribu kutafuta nikaona sipati, nikapata wazo nikaona vitu ambavyo anasema wife yuko navyo, alafu pia ili niwe comfortable zaidi ya kile ninachokifanya, kwa sababu natakiwa ni act kama mke wangu, nikaona kwa nini efort ambayo nataka niiweke kwa mtu mwengine nisiweke wife, kwa hiyo ni kama kutoa kitu mfuko huu na kuhamishia mfuko huu”, alisema Mabeste.

Mabeste anatarajia kuichia video ya wimbo huo kwenye kipindi cha Friday Night Live siku ya Ijumaa ya tarehe 2 Oktoba 2015, ambacho kinarushwa na East Africa Radio/ EATV, na baada ya wiki moja baadae atatoa ya audio na kufanya video ambazo hakuzifanya.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s