Cheka amchapa Mthailand kwa KO,atwaa mkanda wa WBO

Bondia Cosmas Cheka amewatoa kimasomaso watanzania baada ya kushinda mkanda wa Asia Pasific wa WBO kwa kumchapa Bondia wa Thailand,Tewa Tor Surat asubuhi ya leo, nchini Bangkok.

cheka

Cheka alishinda kwa KO katika raundi ya nane na kutwaa mkanda wa WBO uzito wa unyoya kilo 57, mkanda ambao umeipa heshima Tanzania baada ya muda mrefu mabondia wake kupigwa katika mapambao ya nchini Thailand.

Akizungumza na East Africa Radio Katibu Mkuu wa PST Anthony Ruta amesema shirikisho lilijipanga kuhakikisha Cheka anashinda baada ya kuchunguza na kupata ufumbuzi wa mbinu zilizokuwa zikichangia mabondia wa Tanzania kupigwa nchini Thailand, ikiwamo kulishwa vyakula kama vya wanyama wasioliwa ikiwamo nyama ya mbwa na konokono.

Bondia huyo aliondoka mapema wiki hii, akiwa na kocha wake na kiongozi wa shirikisho la masumbwi Tanzania PST na anatarajiwa kurejea jumatatu ijayo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s