Mjengo wa Lulu wadaiwa Kugoma Sokoni

ULE mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambao alimzawadia mama yake Lucresia Karugila, imedaiwa umeshindikana kuuzika baada ya kutangaza kuupiga bei ya shilingi milioni hamsini.

nyumba877

Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa kuupiga bei mjengo huo uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada ya kuona mazingira ya eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua kutofikika kwa urahisi.

“Wamedhamiria kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja kutokana na pesa hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina hadhi.

“Isitoshe ile nyumba ndani inapasukapasuka sakafu huenda kwa sababu ilianza kujengwa siku nyingi, hivyo wateja wengi wanakwamia shilingi milioni 35 wengine milioni 40, pesa ambayo Lulu na mama’ke hawapo tayari kuipokea,” alisema mpashaji huyo.

Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alisema:

“Hii nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni kama kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho, nimeshasema hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia kujenga, nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo mamboº.”

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s