Wenger afurahia ushindi dhidi ya Man Utd

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.

 gun__1443992474_41015-Theo-711

Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa mechi.

“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni binadamu,” alisema.

gun__1443973673_41015-711-Alexis-goal1

“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.”

Arsenal walipata ushindi kupitia mabao mawili ya nyota wa Chile Alexis Sanchez na Mjerumani Mesut Ozil, mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza kwenye mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Emirates.

Kwa meneja wa Manchester United Louis Vvan Gaal, ilikuwa vigumu kukubali matokeo hayo.

„Tulianza vibaya sana, bila kuonyesha ari ya kushambulia na kutaka kushinda. Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kushuhudia hilo katika timu yangu. Sikulitarajia hili,” amesema.

„Unapoipatia timu kama Arsenal mianya tele uwanjani ya kusakata gozi, basi unajua kwamba lazima utashindwa.”

Arsenal na Manchester United sasa zinatoshana alama ingawa Arsenal wako mbele wakishikilia nambari mbili kwenye jedwali kwa wingi wa mabao.

Timu hizo zitarudi mawindoni wiki mbili zijazo mnamo Oktoba 17, baada ya mapumziko ya wiki mbili ya mechi za kimataifa, ambako United watakutaka na Everton uwanjani Goodison Park nao Arsenal wawe ugenini Watford.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s