Chelsea yamtetea Mourinho licha ya masaibu

Chelsea imesema inamuunga mkono meneja Jose Mourinho baada ya klabu hiyo kukumbana na mwanzo mbaya zaidi wa ligi tangu 1978-79.

 150915151948_jose_mourinho_512x288_gettyimages

Klabu hiyo ilijipata nambari 16 ligini ikiwa na alama nane baada ya kulazwa 3-1 na Southampton Jumamosi.

Baada ya kichapo hicho, Mourinho aliambia Sky Sports kuwa klabu hiyo italazimika kumfuta kazi iwapo inataka aondoke.

“Klabu hii ingependa kuweka wazi kwamba Jose anaendelea kuungwa mkono kikamilifu,” klabu hiyo ilisema kupitia taarifa fupi.

“Tunaamini tuna meneja afaaye na awezaye kubadili hali na kwamba ana wachezaji wa kufanya hilo.”

Baada ya mabingwa hao wa Ligi ya Premia kushindwa Jumamosi, Mourinho alisema: “Ninataka kusema wazi. Mwanzo, kwamba mimi si mtu wa kukimbia.

“Pili, iwapo klabu inataka kunifuta lazima inifute lakini mimi sitoroki majukumu yangu au timu yangu.”

151003194409_southampton_chelsea_won_2_512x288_reuters_nocredit

Hayo yakijiri, nahodha wa klabu hiyo John Terry pia amesema Mreno huyo wa umri wa miaka 52 ndiye afaaye Zaidi kusaidia klabu hiyo kujikwamua.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s