Lil wayne adai cash money imemuharibia kwa wasanii wake wa Young Money.

Taarifa za mwisho ambazo zilitoka zilikuwa ni madai ya Lil Wayne dhidi ya Birdman na Cash Money kuiburuza mahakamani kwa kile kilichodaiwa kuwa anaidai Cash Money dola million 51, na kudai kuwa yeye na wasanii wake walishindwa kulipwa.

lil-wayne-tyga-nicki-minaj-young-money-senile-video-shoot9

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ambao ulifanikiwa kupata makablasha ya kesi hiyo na kufanya mahojiano na Weezy, umesema kuwa baada ya kufanya mahojiano na Weezy alisema alipokea barua kutoka kwa Drake, Tyga na Nicki Minaj kwa madai kuwa wamedanganywa na Cash Money juu ya malipo yao.

Pia Nicki Minaj alishawahi kutuma barua ya kulalamika kuwa mtayarishaji wake kulipwa na record Label yake na kwa upande wa Weezy alisema kuwa malipo yote ya wasanii na watayarishaji muziki ni majukumu na wajibu wa Cash Money.

Taarifa Zaidi kutokana na ugomvi mzima ni kuwa Lil Wayne analalamika juu ya pesa za advance millioni 100 ambazo zilitolewa na kampuni ya Universal Music Group kwaajili ya Record Label yake na kuchukuliwa na Cash money bila ya yeye kumfikia.

Aidha kwa upande wa Cash Money inadai ilimpatia Wayne millioni $20 kwa ajili ya wasanii wake mwaka 2012, millioni 12 kwa album yake na millioni $70 kama advances kwa wasanii wake masuala ya masoko pamoja na mambo ya ndani.

Pia CM wanadai wasanii wa Lil wayne walihitajika wawe wametoa album 21 kwa kipindi cha miaka 7 lakini hadi hivi sasa wametoa album 13 tu.

Chanzo: LilWayneHQ.com

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s