Kukosa umoja kunasababisha wizi- Nikki wa pili

Kitendo cha kutokuwa na umoja wa wasanii ambao utatetea maslahi ya wasanii, ni moja ya chanzo cha watu wengine kuiba kazi na mslahi ya wasanii, na kuzorota kwa kazi zao.

Nikki-wa-Pili

Kauli hiyo imetolewa na Msanii Niki wa Pili kutoka lebo ya Weusi, alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio. Niki wa Pili amesema kutokuwepo kwa umoja wa wasanii mambo mengi yatazorota, hivyo ni lazima kuwe na umoja utakaosimama na kuwatetea wasanii.

“Umoja ni kitu cha msingi, kwa sababu bila umoja mambo mengi ya wasanii yatazorota, na kutokuwepo kwa umoja kutatengeneza matundu ambayo wajanja wachache watapitisha mikono yao kwenye hayo matundu na watafaidika nayo, kwa hiyo lazima kuwe na umoja wa wasanii, ambapo utasimama na kuwasemea wasanii”, alisema Niki wa Pili.

Niki wa Pili aliendelea kwa kusema kwamba endapo wasanii hawatakuwa na umoja mambo mengi ya kibiashara yatawashinda kwa sababu umoja wao ndio utakaosimamia biashara zao.

Pia Niki wa Pili amesema wasanii wengi hawaoni umuhimu wa umoja na kutokuwa na msukumo wa kujua kuhusu chamo chao.

“Wasanii wengi pia hawaoni umuhimu wa umoja, kwa hiyo wamekosa msukumo wa kuwa na umoja, na pia chama na chenyewe kimekuwa kimezidiwa sana na kutokuwepo kwa umoja wa wasanii, kwa hiyo kimejikuta nguvu zake zimekuwa chache, lakini umoja ni kitu cha msingi sana, kuna mifano mingi kama wasanii tulivyo ungana tukatoa sauti zetu kwenye katiba tukaona matokeo yake, kwa hiyo mambo mengi ya wasanii yataweza kurekebishwa kukiwa kuna umoja”, alisema Niki.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s