Utafiti: Pilipili huchangia maisha marefu

Kwa miaka mingi sasa, binadamu amekuwa akitumia pilipili kuongeza ladha kwenye mlo wake. Kuna wanaovutiwa na ukali wake na vilevile wanaoichukia kutokana na ukali huo.

 PILIPILI

Sasa utafiti umeonyesha si ladha tu ambayo pilipili huongeza, bali pia hufanya wanaoila kuwa na maisha marefu.

Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida moja la matibabu nchini Uingereza kwa jina British Medical Journal yanasema kula mlo uliotiwa viungo, ikiwemo pilipili, huwa na manufaa kwa afya ya binadamu.

 Pili-pili

Wanasayanasi kutoka Uchina waliangazia afya ya watu takriban laki tano waliojitolea kushirikishwa katika utafiti kuhusu manufaa ya pipili kwa muda wa miaka kadhaa.

Matokeo ya uchunguzi huo yamebaini kuwa wahusika waliokula chakula kilichokuwa na wingi wa viungo, mara moja ama mara mbili kwa wiki walipunguza hatari yao ya kufa kwa asilimia 10.

Viwango vya hatari ya kufariki pia vilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa kwa waliokula vyakula vilivyotiwa vikolezo kwa wingi kila siku.

Katika uchunguzi huo, sehemu kubwa ya viungo kwenye chakula ilikuwa pilipili, na kwa waliokula pipili mbichi walionekana kupunguza hatari ya kufariki kutokana na saratani, ugonjwa wa kisukari na pia maradhi ya moyo.

Mmoja wa walioongoza utafiti huo, Lu Qi,anayesema anapenda sana vyakula vyenye viungo vikali anasema kuna sababu nyingi za manufaa hayo.

“Takwimu hizi zinaonyesha watu wanafaa kula vyakula vyenye viungo Zaidi ili kuboresha afya yao na kupunguza hatari ya kufariki dunia wakiwa wachanga,” alisema Qi, ambaye ni mtaaamu wa lishe katika kitivo cha afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Hata hivyo, anatahadharisha kwamba vyakula vyenye viungo vikali haviwezi kuwafaa watu wenye matatizo ya tumboni kama vile vindonda vya tumbo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s