Kutopata tuzo si kwamba sina kazi nzuri – Barnaba

Msanii Barnaba amesema kutopata tuzo haimaanishi kwamba kazi zake si nzuri, kwani uzuri wa kazi zake mashabiki ndio wanaujua na hiyo kwake ni tuzo tosha

barnabaclassic

Barnaba ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, alipokuwa akifunguka kwa nini hapati tuzo wakati mchango wake katika muziki hata wasanii wenzake wanaukubali.

“Kila kitu kina wakati,wataelewa tu uzuri mashabiki wenyewe wanaelewa nani mtunzi na nani the best, lakini hata anayeshinda au wanaoshinda sio wabaya pia, ni chalenge tu za hapa na pale, unajua thamani ya kitu unachokifanya sio lazima upewe taji, ntahitaji tu kukaa kwenye mioyo ya watu wanaokuamini, kwa hiyo mi naamini i’m the best na hata aliyeshinda pia ni the best, lakini when comes to the truth, ukweli utabaki pale pale tu “, alisema Barnaba.

Barnaba amekuwa mtunzi wa nyimbo mbali mbali zinazofanya vizuri kwenye Bongo Fleva, lakini amekuwa akikosa tuzo kila zinapotolewa na kuishia kuwa nominated, kitendo ambacho kinawashangaza watu wengi hususan wasanii wengi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s