Nguvu ya marafiki ndio ilinibeba – Ben Pol

Kitendo cha Msanii Ben Pol kuondoka kwenye Lebo ambayo ilikuwa inamsimamia, kilimfanya kutojiamini kimuziki, na kukiri kwamba marafiki ndio waliomsaidia mpaka kufanikiwa.

Capture%20(1)

Ben Pol ambaye anafanya vizuri kwenye upande wa R&B, amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio, na kueleza kwamba marafiki walisukuma kazi zake na kuzifanya zitambulike nchi nzima na kumpatia tuzo.

“Mimi nilivyotoka kwenye lebo mwaka 2011, nilikuwa sina confidence ya kusema kwamba nitaweza kufanya muziki mwenyewe, sina record label, lakini marafiki zangu wachache waliokuwa wanasikiliza nyimbo zangu na wengine ambao walikuwa kwenye media, walikuwa wanatumia nguvu yao kubwa sana kuwahamasisha watu kwamba huu muziki ni mzuri, na kupitia nguvu yao ikabadilisha ikawa kitu kikubwa nchi nzima mpaka na sehemu za karibu zote watu wakawa wanasapoti”, alisema Ben Pol.

Ben pol aliendelea kusema kwamba kitendo hicho ndicho kilimfanya aweze kutwaa tuzo ya wimbo bora wa R&B mwaka 2012, kitu ambacho kilimshangaza hata yeye mwenyewe.

“mpaka mwaka 2012 nashinda tuzo ya wimbo bora wa R&B niko nyumbani naangalia tuzo kwenye Tv, kwa sababu najua naweza nisipate kwa sababu sina record label, lakini nikasema Kaa!!?? nimeshinda mimi tena!? nimekaa na marafiki tu”,alisema Ben Pol kwenye Show ya Plane Bongo.

Pia Ben Pol amewataka wasanii wenzake kufanya kazi nzuri kwani kazi nzuri zinajiuza zenyewe.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s