Raia wa India atengeneza gari kubwa duniani

Mchoraji wa miundo ya magari nchini India Sudhakr Yadav amejaribu kuweka rekodi ya pili ya Guiness kwa kutengeneza gari analotumai litakuwa ndilo kubwa zaidi duniani.

 151008115808_largest_car_640x360_bbc_nocredit

Gari hilo, ambalo limeundwa likifanana na gari aina ya Ford Toure lililoundwa mwaka 1922, lina urefu wa futi 26 (mita 8) kwenda juu na ukubwa wa futi 50 lina ukubwa maradufu wa basi lililo na ghorofa mbili mjini London.

Bwana Yadav tayari anashikilia rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuwa na baiskeli ndefu zaidi duniani.

Mchoraji huyo wa miundo ya magari anamiliki makavazi ya magari katika mji wa Hyderabad ulioko kusini mwa India ambapo anaonyesha mitindo tofauti ya magari.

151008115832_largest_car_2

Magari hayo yana maumbo na ukubwa tofauti .

”Tunalenga kuvunja rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuunda gari kubwa duniani. Ni rekodi mpya na nina matumaini nitaipata,” alisema.

Anatarajia gari hilo liwe na mngurumo sawa na wa magari ya mbio za langalanga au Formula One.

Baiskeli yake ya magurudumu matatu ni ndefu zaidi ya gari hilo ikiwa na futi 41.5 kwenda juu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s