Pacquiao kupigana mara ya mwisho

Bondia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa akastaafu katika ulingo wa ndondi baada ya pigano moja mwaka ujao.

 150503075031_mayweather_pacquiao_wbo_hug_624x351_afp

Pacquiao,ambaye alipoteza kwa Floyd Mayweather katika pigano la mwisho ,anataka kuwania kiti kimoja katika bunge la seneti mwaka 2016.

Raia wa Uingereza Amir Khan ni mmoja ya wapinzani wa Pacquiao mwenye umri wa miaka 36,huku Terence Crwaford kutoka Marekani akiwa mpinzani mwengine.

”Nadhani niko tayari.Nimepigana ndondi kwa zaidi ya miaka 20”,bingwa huyo wa dunia katika uzani 6 tofauti aliambia ANC.

”Unapokuwa seneta,lengo lako linakuwa kazi yako na familia,Nitahitajika kuwacha mambo mengine ambayo yanahitaji kupewa kipaumbele”

150506030200_sp_pacquiao_640x360_ap_nocredit

Pacquiao amesema kuwa ”hawezi kusema” iwapo pigano lake la mwisho litakuwa dhidi ya Mayweather,baada ya raia huyo wa Marekani kuahidi kustaafu baada ya ushindi wake dhidi ya Andre Berto.

Raia huyo wa Ufilipino ,ambaye alifanyiwa upasuaji katika bega lake baada ya pigano lake na Mayweather,anajivunia rekodi ya mapigano 57,kushindwa mara 6 na sare ya mapigano 2.

Chanzo: Bbcswahili.com

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s