Pharrel Williams atangaza kumsapoti Hilary Clinton

Pharrel Willliams ametoa taarifa hiyo alipokuwa akihojiwa kwenye moja ya vipindi vya television nchini Marekani, na kusema kwamba ni wakati wa mwanamke kuongoza nchi hiyo kwani wanawake hufikiria mambo kwa njia ya kipekee.

pharrel-williams

Wakati hapa nyumbani tukishuhudia wasanii mbali mbali wakiwapigia kampeni baadhi ya wagombea urais mwaka huu, huko Marekani pia hali imekuwa kama hii ambapo leo msanii Pharrell Williams ameamua kutangaza kuwa anamsapoti Bi. Hilary Clinton kwenye kinyang’anyiro cha urais kinachoendelea nchini Marekani kwa sasa.

“Ni muda wa mwanamke kuwa pale, wanawake wanafikiria vitu kwa umakini na kwa uchambuzi zaidi na sio kibinafsi, nasema nafurahi kuwa mwanaume lakini nawapenda wanawake, kwamba kama tuna mtu wa kuangalia nchi yetu , anyefikiria vitu kwa ujumla, alisema Pharel.

Pharrel Williams ambaye alikuwa kwenye kipiindi hicho cha televisheni na kutumbuiza wimbo wake wa freedom, amesisitiza akisema kwamba si kama hampendi rais wa sasa, isipokuwa ni zamu ya Bi. Hilary Clinton.

“Si kama simpendi rais wetu wa sasa, najisikia kama ni zamu ya Hillary, watu wako kama wanahitaji rais ambaye tutacheza naye, lakini huyo siye atakaye tatua matatizo yako, unahitaji mtu atakee yachukulia kwa uzito” alisema Pharrel.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s