Wastara Atishiwa Kuuawa!

atari! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadai kutishiwa maisha kwa kutumiwa  ujumbe wa WhatsApp na ustaadhi ambaye aliwahi kutangaza kutaka kumuoa, jambo lililosababisha staa huyo kuamua kumfungulia mashtaka.

WASTARA6

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wastara alifunguka kuwa kutokana na vitisho anavyotumiwa na ustadhi, hivyo akitua Dar kutoka mikoani atakwenda kumfungulia mashtaka kituo cha polisi kwani vitisho hivyo vinahatarisha usalama wake.

“Hebu fikiria mtu ananiandikia ujumbe kuwa atahakikisha nimeua ndiyo ataniacha, ina maana yale yanayonitokea ni yeye ananisababishia!” alisema Wastara.

Wastara alimtumia mwandishi ujumbe wa ustadhi huyo unaosomeka; ‘na bado siyo unatamani kuua na utaua, nitahakikisha umeua ndiyo na mimi nakuacha’.

Vitisho vya jamaa huyo vinakuja baada ya gazeti dada la hili, Ijumaa linalotikisa mitaani kila Ijumaa kuandika habari ya Wastara iliyosikitisha ambayo staa huyo alielezea namna anavyopatwa na hasira na kutaka kuua mtu ndipo  ustadhi huyo akamjibu kwa ujumbe huo.

Ustadhi huyo aliwahi kuripotiwa na gazeti ndugu na hili, Risasi kuwa ana tatizo la kumsema Wastara hata awapo katikati ya swala, jambo lililomfanya awatafute waandishi ili wamsaidie kumuunganisha na mwigizaji huyo akitaka kumuoa lakini mwanadada huyo alidaiwa kumtolea nje.

Chanzo:GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s